Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa WTO: Uchumi wa Dunia umenufaika kutokana na China kujiunga na WTO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 14, 2021

Katika mahojiano na Gazeti la Le Monde la Ufaransa, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Pascal Lamy amesema kwamba, kujiunga na Shirika la Biashara Duniani kwa China kumeongeza ukuaji wa uchumi wa Dunia, na uchumi wa Dunia umenufaika kutokana na China kujiunga na WTO.

Kwa mujibu wa Gazeti la Le Monde la Ufaransa, Lamy alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani kutoka Mwaka 2005 hadi Mwaka 2013 na alishiriki kwenye mazungumzo kuhusu China kujiunga na Shirika la Biashara Duniani. Lamy amesema, China ilifanya kazi nyingi ili kujiunga na WTO na China imepunguza kwa kiasi kikubwa ushuru wa uagizaji bidhaa.

Lamy anaamini kuwa China kuagiza vifaa na teknolojia kutoka nchi za nje kumeufanya uchumi wake kuwa bora na imara, na wanunuzi bidhaa wa sehemu mbalimbali duniani wamenufaika pia na bidhaa zenye bei nafuu zaidi kutoka China.

Akizungumzia mustakabali wa Shirika la Biashara Duniani, Lamy amesema kuwa, katika miaka 20 iliyopita tangu China ijiunge na WTO, baadhi ya kanuni za shirika hilo zimebadilika, lakini mfumo wa pande nyingi wa majadiliano hauwezi kubadilika.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha