

Lugha Nyingine
Toleo la Pili la Mwongozo wa kukabiliana na UVIKO-19 wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 watolewa
Nembo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 (Kushoto) na Nembo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing 2022. (Kamati ya maandalizi ya Beijing 2022/Kutolewa kupitia Xinhua)
BEIJING - Ikiwa imesalia chini ya miezi miwili kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kuanza, Kamati ya Maandalizi, pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) zimechapisha toleo la pili la mwongozo juu ya hatua za kukabiliana na UVIKO-19 wakati wa michezo hiyo.
Kama ilivyokuwa kwa toleo la kwanza, toleo la pili pia limetoa matoleo tofauti kwa wanariadha na maafisa wa timu, pamoja na wahusika wengine, ikiwa ni pamoja na Familia za Olimpiki na Paraolimpiki, vyombo vya habari, Mashirikisho ya Kimataifa (IFs) na wafanyakazi kwa kawaida.
Mambo mapya yaliyoongezwa kwenye toleo la pili ni pamoja na taarifa zilizotakiwa moja kwa moja na wadau na maoni yaliyopokelewa wakati wa mikutano mbalimbali iliyofanyika tangu Oktoba mwaka huu, pamoja na taarifa za ziada kuhusu chanjo; matakwa ya kuingia mipaka ya China; ukataji tiketi za ndege; kupima virusi vya korona kabla ya kuondoka; kipindi cha kabla ya Michezo; mfumo wa kitanzi kilichofungwa; malazi; usafiri; chakula na vinywaji; upimaji na uchunguzi wa afya; ufuatiliaji wa afya; usimamizi wa watu waliokutana na watu wenye UVIKO-19; na kipindi kati ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu (Paralympic).
Sehemu ya "Mambo Muhimu ya kukumbuka" pia imejumuishwa ili kusaidia kuwaongoza wahusika kupitia kila hatua ya uzoefu wa muda wa michezo hiyo.
"Hatua zilizoainishwa katika toleo la pili la mwongozo zimeandaliwa kwa mujibu wa utafiti wa hivi punde wa kisayansi wa UVIKO-19, maoni ya wataalam na uzoefu wa mashindano mengine ya kimataifa," ameeleza Naibu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Kamati ya Maanzalizi ya Michezo ya Omlimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, Han Zirong.
Kwa upande wake Christophe Dubi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki (IOC), amesema kuwa hatua hizi za kukabiliana na UVIKO-19, zimewekwa baada ya kushauriana na wataalam wakuu wa afya duniani, ni muhimu kwa usalama na mafanikio ya michezo hiyo.
"Kwa kutoa mazingira salama, hii itatoa uzoefu wa kipekee wa wakati wa michezo, na kusaidia wanamichezo kuzingatia kikamilifu misingi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu” amenukuliwa akisema.
Naye Colleen Wrenn, Afisa Mkuu wa Ufanikishaji wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC), amesema: "Kwa uzoefu uliopatikana katika uandaaji wa mashindano makubwa ya michezo duniani kote na maoni ya wataalam wa matibabu, tuna uhakika hatua zilizoainishwa katika kitabu cha mwongozo zitaruhusu washiriki kushiriki katika Michezo ya Majira ya Baridi ya Olimpiki na Walemavu huku wakilinda afya zao. Cha muhimu zaidi ni mwongozo wa Michezo umeandaliwa ili kulinda afya ya washiriki wote na watu wa China."
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itafanyika kati ya Februari 4 na 20, 2022, na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu itafanyika kuanzia Machi 4 hadi 13.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma