

Lugha Nyingine
Xinjiang yazungumza: Uhuru wa imani ya kidini unastawi
URUMQI - Akiwa amevalia gauni jeupe na glavu za plastiki, Yulidus Abulimit alikuwa akiangalia kwa makini hali ya vitabu. Kutokana na kurasa hizo zilizokunjamana na za manjano, si vigumu kusema kwamba baadhi ya vitabu hivyo ni vya zamani zaidi kuliko binadamu yeyote aliye hai.
Huu ni utaratibu wake wa kila siku wa kufanya kazi katika ofisi ya vitabu vya kale ya kamati ya Masuala ya Kikabila ya Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. Ofisi hiyo imekusanya zaidi ya nakala 2,000 za kale za vitabu vya kale vya Kiislamu katika lugha za Kiarabu, Kiajemi na nyinginezo.
"Mswada huu uliandikwa tangu mwishoni mwa karne ya 19," anasema Yulidus Abulimit akiwa na nakala ya Quran. "Karatasi hiyo ni gome la mti wa mforsadi na kifuniko kimetengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe."
Kisha akaonesha kitabu kikongwe zaidi katika mkusanyiko wao wa sasa - "Wasifu wa Nabii" chenye historia ya miaka 230, ambacho kimejumuishwa katika orodha ya Vitabu Adilifu ya Kitaifa vya China.
Xinjiang imefanya jitihada kubwa za kuhifadhi na kulinda maandishi ya kidini, kwa kutengewa fedha maalum na serikali. Mwaka1983, kikundi cha uongozi kilianzishwa katika eneo hilo kwa ajili ya kukusanya, kuhifadhi na kuchapisha vitabu vya kale vya makabila madogo.
Yulidus Abulimit anasema kuwa serikali kuu na za mkoa zimetilia maanani kazi hiyo kwa miaka mingi. "Tumepanga zaidi ya wataalam na wasomi 200 kukusanya, kupanga na kufufua vitabu vya kale vya kidini katika zaidi ya maeneo 60 kote mkoani Xinjiang," anaongeza.
Maktaba maalum yenye halijoto na unyevunyevu zisizobadilika imejengwa huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa wa Xinjiang kwa ajili ya kuhifadhi vitabu vya kidini vilivyoko hatarini kutoweka na vya thamani, na mpango wa kuweka kidijitali vitabu vya kale vya kidini pia umezinduliwa ili kuvifanya vipatikane zaidi.
Subatjan Semi, mwenye umri wa miaka 22, ana ndoto za kuwa Imam, kama babu yake. Mnamo Mwaka 2019, alihitimu kutoka shule ya sekondari na kuanza masomo katika Chuo cha Kiislamu ya Xinjiang, ambacho kinachukuliwa kuwa chuo bora zaidi cha Kiislamu katika eneo hilo.
Subatjan Semi huchukua kozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qurani, masuala ya kidini, lugha ya Kiarabu, Kichina, historia na utamaduni. "Kuna wanafunzi wa makabila ya wauygur, wakirgiz na wakazak katika darasa letu. Walimu na wanafunzi wanaishi kwa masikilizano," anasema.
Kwa mujibu wa Kamaldin Ahmat, profesa msaidizi katika taasisi hiyo, hivi sasa kuna zaidi ya wanafunzi 1,100 katika chuo hicho, huku wanafunzi wapya wakiandikishwa kila mwaka.
Kwa mujibu wa waraka ulitolewa na Serikali Mwezi Julai mwaka huu, Xinjiang inalinda kikamilifu shughuli halali za kidini na inahakikisha uhuru wa umma wa imani ya kidini kwa mujibu wa sheria. Njia za waumini kupata ujuzi wa kidini zimehakikishwa. Vifaa na mazingira ya maeneo ya kidini yameboreshwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma