

Lugha Nyingine
Sekta binafsi ya Tanzania kuimarisha ushiriki wa watanzania wanaoishi nchi za nje katika shughuli za kiuchumi
DAR ES SALAAM – Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Watanzania wanaoishi nchi za nje (TDH) zimetia saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) ili kuimarisha ushiriki na ushirikishwaji wa watu hao katika shughuli za kiuchumi.
Taarifa iliyotolewa Jumatano wiki hii na TPSF mjini Dar es Salaam inaeleza kwamba hatua hiyo inalenga kuwapa fursa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweka mitaji yao katika miradi ya uwekezaji, kukuza uhusiano wa kibiashara na uanzishaji wa viwanda, na kukuza diplomasia ya uchumi kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Francis Nanai ametangaza katika taarifa hiyo kwamba Watanzania 40 wanaoishi nchi za nje wamewasili Tanzania na wana nia ya kuwekeza nchini humo.
Taarifa hiyo imetaja maeneo yaliyokusudiwa kuwekezwa kuwa ni viwanda vya kusindika mkonge, kilimo cha kibiashara, madini, viwanda vya kusindika chakula, nishati na ufugaji wa samaki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TDH, Nassor Basalama, amesema wananchi wanaoishi nchi za nje pia wana nia ya kuwasaidia Watanzania kupata fursa za masomo nje ya nchi na kutangaza vivutio vya utalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma