“China ina uzoefu wa kutosha wa kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 17, 2021

Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 ukioneshwa kwenye ziara ya Maonesho ya Mwenge kwenye Bustani ya Shougang, Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 13, 2021. (Xinhua/Zhang Chenlin)

KIEV - Sergey Bubka, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Ukraine (NOC) amesema kwamba China ina uzoefu wa kutosha wa kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022, ambayo itakuwa muhimu katika kukabiliana na changamoto na kuimarisha mshikamano duniani kote.

Amesema "China ina uzoefu mkubwa sana wa kuandaa Michezo ya Olimpiki. Ina vifaa vizuri, ina uzoefu, inajua la kufanya," Bubka ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano Jumatano ya wiki hii. Na ameongeza kwamba, Michezo ya Olimpiki ni ya binadamu wote na ni mambo zaidi ya siasa, dini na mipaka.

"Haijalishi [kama kuna] maslahi ya kisiasa, dini, hakuna mipaka, sisi ni binadamu. Na kupitia Olimpiki, kupitia maadili ya Olimpiki tunaleta kila mtu pamoja," amesema.

Bubka amesema, Michezo ya Majira ya Baridi ya Olimpiki ya Beijing 2022 itakuwa chombo muhimu cha kuelezea mshikamano wa jumuiya ya kimataifa dhidi ya janga la UVIKO-19.

"Nadhani kwa wakati huu, kipindi cha UVIKO-19, ni muhimu sana kufanya Michezo ya Olimpiki," amesema.

Kwa mujibu wa Bubka, Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 itatuma ujumbe mzuri kwa ulimwengu kwamba binadamu watashinda janga hili kupitia juhudi za pamoja.

"Tutashinda changamoto hii ya UVIKO-19 na bila shaka lazima tuwe pamoja," Bubka amebainisha.

Akizungumzia mipango ya Ukraine katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, Bubka amesema kuwa maandalizi ya mwisho yanaendelea vizuri.

"Ni kipindi muhimu sana kwa wanamichezo wanaojiandaa na Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Bila shaka, wanafanya mazoezi, wameanza mashindano tayari, kipindi hiki ni muhimu kwa wanamichezo wetu kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki," amesema.

Kwa mujibu wa Bubka, Ukraine inatarajia kutuma ujumbe wa watu 100, wakiwemo wanamichezo 40 hadi 46, kwenda Beijing.

Bubka ambaye alikuwa Bingwa wa Olimpiki wa mbio za nyika kwa wanaume Mwaka 1988, amesema ametembelea China mara nyingi na amevutiwa na uzuri wa nchi hiyo na urafiki wa watu wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha