Dondoo Muhimu za Olimpiki ya Majira ya Baridi: Ni mashindano gani mapya ya Michezo ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2021

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 imepangwa kujumuisha jumla ya mashindano 109 ya medali, na saba kati ya mashindano hayo ni mapya kwa Michezo ya Majira ya Baridi.

Mashindano saba mapya yatajumuisha mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa ubao kwa wanawake na kuteleza kwenye barafu kwa ubao kwa wanaume na wanawake mtindo huru, pamoja na mchezo wa mbio za kupokezana za njia fupi za kuteleza kwenye barafu kwa kasi, mchezo wa kuteleza kwenye barafu kwa ubao na kuruka juu, mashindano ya ustadi wa kuteleza kwenye barafu kwa mtindo huru, na mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa ubao kwa kuvuka vikwazo.

Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Li Lingwei alisema kuwa matukio hayo saba yameongezwa hivi karibuni kwa sababu hayahitaji kumbi mpya za kujengwa, na watangazaji wa TV pia wanamipango ya kutangaza idadi kubwa ya mashindano wakati wa Michezo ya Majira ya baridi.

Li aliongeza kwamba, kando na hilo, mashindano haya mapya yanajulikana zaidi miongoni mwa vijana na yatasaidia kuboresha zaidi kiwango cha ushiriki wa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha