Lugha Nyingine
Xi asisitiza kukamilisha kanuni za Chama ili kulinda uongozi wa Chama katika utawala wa nchi
Wang Huning, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akitoa hotuba kwenye mkutano wa kitaifa kuhusu kazi ya kanuni za ndani za CPC mjini Beijing, Desemba 20, 2021. (Xinhua/Pang Xinglei)
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza jukumu muhimu la kanuni za ndani za CPC katika kudumisha uongozi wa Kamati Kuu ya CPC katika utawala wa nchi.
Xi Jinping ameyasema hayo kwenye mkutano kuhusu kazi ya kanuni za ndani za CPC uliofanyika Jumatatu ya wiki hii Beijing, ambapo amesisitiza kwamba, kanuni hizo ni muhimu kwa utawala wa nchi wa muda mrefu wa CPC na ustawi wa kudumu na utulivu wa nchi.
Akibainisha maendeleo makubwa katika kuimarisha kanuni za Chama tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, Xi amesisitiza juhudi zaidi za kutekeleza kwa hiari na kwa uthabiti utawala unaozingatia kanuni juu ya CPC na kukamilisha kanuni za ndani ya Chama hicho.
Amesema, majukumu makuu ya kanuni za ndani za CPC yanapaswa kutekelezwa vyema ili kuhakikisha uongozi thabiti wa Chama katika kudumisha na kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China.
Wang Huning, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba.
Akibainisha kwamba maagizo ya Xi yamezingatia ustawishaji wa Taifa la China na mabadiliko makubwa yanayotokea duniani, Wang amesema sera za Kamati Kuu ya CPC na maagizo ya Xi lazima yatekelezwe kikamilifu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma