China yaongeza juhudi kuharakisha mageuzi na kufungua mlango

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2021

Picha iliyopigwa Januari 14, 2021 ikionesha mwonekano wa usiku wa Lujiazui, eneo la Pudong, mji wa Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

BEIJING - China iko mbioni kuwa nyanda mpya katika mageuzi na ufunguaji mlango.

Juhudi za nchi hiyo katika sekta hiyo ni Dhahiri. Mji wa Kusini wa Shenzhen unajenga eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, Mkoa wa Hainan unajenga Bandari ya Biashara Huria (FTP), na Pudong ya Shanghai inatangulia katika ujenzi wa kisasa wa Ujamaa.

Mageuzi na Uvumbuzi

Mwezi uliopita, kampuni nne za Shanghai zilipokea leseni za kwanza za biashara kulingana na utaratibu mpya wa kuruhusiwa kuingia kwenye soko.

Xu Wei, Meneja Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya kitamaduni yenye makao makuu yake mjini Shanghai, ZiLiHangJian, anasema chini ya utaratibu wa zamani, wakati walitaka kufungua duka la vitabu lenye huduma ya kahawa na chakula katika eneo la Biashara Huria la Shanghai, walipaswa kutumia muda mrefu kuomba leseni tofauti za mgahawa na uchapishaji.

"Sasa leseni za sekta mbalimbali zimeunganishwa na kuwa moja, tunaweza kuanza biashara yetu kwa haraka zaidi," anasema Xu.

Hii ni mojawapo ya hatua za hivi punde za Pudong ya Shanghai kuboresha zaidi mazingira ya biashara katika juhudi zake za kuongoza kwenye ujenzi wa kisasa wa Ujamaa China.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa Mwezi Julai mwaka huu, Pudong itatafuta namna ya kujaribu utaratibu wa usajili wa biashara na utaratibu wa kuruhusu kuingia sokoni, na kutayarisha hatua maalum za kurahisisha kuingia sokoni.

Shenzhen, ambayo ilianza ujenzi wa eneo la kielelezo cha Ujamaa wenye umaalumu wa China mnamo Agosti 2019, imepitisha hatua kadhaa za mageuzi na uvumbuzi.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Shenzhen imepitisha sheria na kanuni mpya 17 zinazohusisha eneo maalum la kiuchumi na nyingi ya hizo ni za kwanza nchini China.

Kupanua Ufunguaji wa Mlango

Benki ya HSBC ilifungua tawi lake huko Haikou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Hainan Kusini mwa China, Desemba 6 mwaka huu, na kuwa benki ya kwanza ya kimataifa kufungua shughuli zake mkoani Hainan tangu kujengwa kwa Bandari ya Biashara Huria (FTP).

Mark Wang, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HSBC Bank (China) anasema kwamba, ikiwa lango muhimu la kufungua mlango kwa China, bandari ya biashara huria ya Hainan ni mojawapo ya mifano ya kuigwa ya China kuendelea kufungua soko lake na kujiunga kwa kina katika uchumi wa Dunia, na inajitahidi kuwa kituo muhimu cha mzunguko wa pande mbili juu ya msingi wa hadhiya kijiografia na sera.

Tangu China ilipotangaza mpango wa kuijenga Hainan kuwa Bandari ya Biashara Huria Mwezi Juni mwaka jana, Hainan imekuwa mahali muhimu kwa kampuni za kimataifa kuwekeza nchini China.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa jumla ya kampuni 1,649 za nchi za nje zimeanzisha biashara zao mjini Hainan katika kipindi cha miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, ambayo ni ongezeko la takriban asilimia 153.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo, huku uwekezaji kutoka nchi za nje unaotumika ukifikia takriban dola za kimarekani Bilioni 3, ikiwa ni ongezeko la asilimia 414.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Manunuzi ya bidhaa zisizo na ushuru ni mojawapo ya sera za msingi za Hainan FTP, na chapa nyingi za kimataifa zimeingia kwenye soko la manunuzi ya bidhaa zisizo na ushuru huko Hainan mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kwa pamoja na Taasisi ya Mahesabu ya Kifedha ya KPMG China na Ripoti ya Moodie Davitt Mwezi Mei mwaka huu, sera ya manunuzi iliyoimarishwa mnamo Julai 2020 ilitoa msukumo mkubwa kwa utalii wa kimataifa na soko la rejareja.

Tangu tarehe 1 Julai 2020, Hainan imeongeza kikomo cha manunuzi ya bidhaa zisizo na ushuru kwa kila mtu kutoka yuan 30,000 (takriban dola za Marekani 4,709) hadi yuan 100,000 kila mwaka. Kikomo cha awali cha bidhaa zisizotozwa ushuru cha yuan 8,000 kwa bidhaa moja pia kimeondolewa. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha