Hekalu la Kwanza la Shaoling Lazinduliwa Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2021

Picha iliyopigwa tarehe 22, Desemba, 2021 ikionesha muonekano wa Hekalu la Shaolin wa Lusaka wa Zambia. (Xinhua/Martin Mbangweta)

Ili kuwaonesha Wazambia Kungfu ya China na utamaduni wa China , hekalu la kwanza la Shaolin limezinduliwa huko Lusaka, Zambia.

Hekalu hilo lilianzishwa na Hekalu la Shaolin la Mlima Song la China pamoja na Kampuni ya Hua’an ya China nchini Zambia.

Mwalimu Mkuu wa Hekalu hilo Yan Lun alisema, mradi huo unalenga kutoa mafuanzo ya Kongfu ya Shaoling na utamaduni wa China , kuwasaidia Wachina kujua utamaduni wa Afrika, na kukuza urafiki kati ya China na Afrika

Ujenzi wa hekalu hilo ulianzishwa Aprili, 2019, na ulikamilika Mwezi Julai, 2021. Masufii wanne kutoka Hekalu la Shaolin la Mlima Song la China wanahubiri kwenye hekalu hilo jipya.

Na pia hekalu hilo linataka kuwasaidia makundi ya watu wenye hali dhaifu kwenye jamii. Hivi sasa, linawatunza watoto watatu yatima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha