Uongozi wa CPC wasisitiza kuimarisha imani ya kihistoria, umoja, roho ya mapambano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2021

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akiongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na kutoa hotuba muhimu. Mkutano wa kukosoa na kujikosoa, wenye kaulimbiu ya kusoma historia ya Chama, umesisitiza kuendeleza misingi ya kuanzishwa kwa CPC na kushikilia uzoefu wake wa kihistoria kutokana na juhudi katika karne iliyopita. Mkutano ulifanyika kuanzia Desemba 27 hadi 28. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umesisitiza kuimarisha imani ya kihistoria ya wanachama wa CPC, umoja na moyo wao wa mapambano.

Mkutano huo wa siku mbili wa kukosoa na kujikosoa, wenye mada kuhusu kusoma historia ya Chama, umesisitiza kuendeleza misingi ya kuanzishwa kwa CPC na kushikilia uzoefu wake wa kihistoria kutokana na juhudi katika karne iliyopita.

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, ameongoza mkutano huo uliomalizika Jumanne ya wiki hii na kutoa hotuba muhimu.

Mkutano huo ulipitia Ripoti ya utekelezaji wa maamuzi manane ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC katika Mwaka 2021, pamoja na ripoti nyingine ya kushughulikia hali ya urasimu katika utekelezaji wa taratibu kwa ajili ya kupunguza mzigo wa kazi katika ngazi ya shina Mwaka 2021.

Baadaye, wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC walihutubia mmoja baada ya mwingine, wakitoa ukosoaji na kujikosoa.

Mkutano huo umesisitiza kuwa 2021 ni mwaka wenye umuhimu wa kimnara katika historia ya CPC na nchi.

China imeendelea kupanga mpango na kufanya uratibu katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi na udhibiti wa janga la UVIKO-19, huku ikiratibu maendeleo makubwa katika nyanja zote za shughuli za CPC na usalama wa nchi. Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano umeanza vema.

Wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC wameona kwa kauli moja kwamba kubainisha nafasi ya msingi ya Komredi Xi Jinping kwenye Kamati Kuu ya CPC na katika Chama hicho kwa ujumla, na kubainisha nafasi ya kiuongozi ya Mawazo ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya ni ya umuhimu madhubuti wa kuendeleza mchakato wa kihistoria wa ustawishaji wa taifa la China.

Mkutano huo umeeleza, miaka 100 iliyopita ya CPC imeonesha kwamba kushikilia kwa uthabiti msingi wa Kamati Kuu ya CPC na Chama kizima ni jambo la msingi kwa CPC kukusanya maoni ya pamoja na kufanya uamuzi madhubuti katika nyakati ngumu, na kunatoa uhakikisho muhimu kwa CPC kuendelea kwa utulivu katika mshikamano na umoja.

Katika hotuba yake, Xi amefanya majumuisho kuhusu kauli za kujitathmini za wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya CPC.

Xi amesisitiza kuwa CPC daima imekuwa ikizingatia umuhimu wa elimu juu ya historia ya chama.

Xi amesema, Kadiri chama kinavyojikusanyia hekima ya kihistoria, ndivyo kitachukua hatua kubwa zaidi kudhibiti mustakabali wake.

Amebainisha kuwa kampeni ya kusoma historia ya CPC iliyoanzishwa na Kamati kuu ya Chama mwaka huu ndani ya CPC na katika jamii nzima inalenga kuongeza imani katika historia na kuimarisha mshikamano na umoja.

Xi amebainisha kwamba, tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012, umoja na mshikamano wa CPC, ambao ndiyo nguzo ya Chama, umefikia kiwango kipya kutokana na juhudi za pamoja za Chama kizima.

Xi ameongeza kwamba, Kamati Kuu ya CPC iliamua kuangazia zama mpya za ujamaa wenye umaalum wa China katika azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Sita wa Kamati Kuu ya 19 ya CPC, ambalo lina umuhimu mkubwa kwa Chama katika kuunganisha fikra na vitendo kuhusu maswali makuu ya kinadharia na vitendo

Amebainisha kwamba, kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ni jukumu kuu la kisiasa la Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya CPC kwa mwaka ujao.

Xi amesisitiza kwamba, wakati wa uchaguzi na mabadiliko ya viongozi, viongozi katika nafasi za uongozi lazima wafuate kikamilifu nidhamu na sheria husika. Amehimiza juhudi za kuwaelimisha na kuwaongoza viongozi kubeba picha kubwa akilini na kuzingatia kutekeleza majukumu yao. 

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akiongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na kutoa hotuba muhimu. Mkutano ulifanyika kuanzia Desemba 27 hadi 28. (Xinhua/Ju Peng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha