Dondoo za Olimpiki ya Majira ya Baridi: Je! ni idadi gani ya wanamichezo wa kike katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2021

Jumla ya wanamichezo 2,892 wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya michezo huko Beijing Mwaka 2022, kati yao, 1,314 ni wanawake, ambayo imechukua asilimia 45.2. Asilimia hiyo ya wanamichezo wanawake, ndiyo ya juu zaidi katika historia ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi.

Mchezo gani ni wa wanaume pekee kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi?

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imepangwa kuwa na matukio ya michezo 109 kwenye zaidi ya sehemu 15 katika michezo saba. Miongoni mwa matukio hayo ya michezo, moja tu ni kwa ajili ya wanamichezo wa kiume pekee, ambalo ni la mchezo wa biathlon ya Nordic.

Ingawa kwa sasa wanawake hawawezi kushiriki katika mchezo wa biathlon, ambao unajumuisha kuteleza kwenye theluji porini na kuruka juu ya theluji katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, wanakaribishwa kushiriki katika mchezo huu katika mashindano mengine makubwa kama vile Kombe la Dunia na Kombe la Mabara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha