Dondoo za Olimpiki ya Majira ya Baridi: Je, kuna mwanamichezo ambaye ameshinda medali ya dhahabu katika Olimpiki ya Majira ya joto na Majira ya baridi?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2021

Si vigumu kupata mwanamichezo ambaye ameshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto na Majira ya baridi; lakini kazi ngumu ni kupata mmoja ambaye ameshinda medali ya dhahabu katika matoleo yote mawili ya michezo ya olimpiki. Kwa hakika, mwanamichezo wa Marekani Edward Eagan ndiye mtu pekee hadi sasa ambaye ameshinda medali za dhahabu kwenye Olimpiki ya Majira ya joto na ya baridi.

Eagan alikuwa bingwa wa ndondi kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Antwerp Mwaka 1920. Kisha miaka 12 baadaye, kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Lake Placid Mwaka 1932, alishinda tena medali ya dhahabu kwa wachezaji wanne wa bobsled (mchezo wa kuteleza na kigari kwenye barafu), ambapo kabla yake alikuwa amefanya mazoezi kwa wiki tatu tu.

Mafanikio ya Egan hayakuwa tu kwenye uwanja wa michezo. Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Harvard na Chuo Kikuu cha Yale, na baadaye akaendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Oxford. Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alikuwa kanali wa Jeshi.

Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa wanamichezo siku hizi kurudia muujiza wa Eagan kwenye Michezo ya Olimpiki kwani kadri uwezo wao unavyoimarika na ushindani unakuwa mkali zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha