Mkoa wa Hebei nchini China waanza kuboresha kampuni 1,000 ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2022

Picha iliyopigwa Tarehe 26 Julai 2021 ikionesha mandhari ya mradi wa Tangshan Huahai, mji wa Tangshan, Mkoa wa Hebei Kaskazini mwa China. (Xinhua/Mu Yu)

SHIJIAZHUANG - Mkoa wa Hebei Kaskazini mwa China utachunguza takriban kampuni 1,000 zenye matumizi ya juu ya nishati na utoaji mwingi wa hewa ya kaboni ili kuziboresha na kuzifanya kuwa rafiki kwa mazingira.

Idara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya mkoa huo inatarajia kwamba, teknolojia za kiwango cha juu za uzalishaji, mbinu na vifaa vitatumika wakati wa mchakato wa kuboresha kampuni hizo zinazokabili uchafuzi wa mazingira.

Kampuni kubwa za chuma, saruji, na vioo bapa za mkoa huo zinatakiwa kujijengea viwanda vilivyo rafiki kwa mazingira katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kama sehemu ya Utekelezaji wa Mpango wa 13 wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016-2020), Mkoa wa Hebei umefanikiwa kupunguza zaidi ya tani milioni 82 za uwezo wa kuzalisha chuma, takriban tani milioni 12 za uwezo wa uzalishaji wa saruji na tani milioni 2.5 za uzalishaji wa kioo bapa.

Idara hiyo imeongeza kwamba, Hebei imejenga viwanda 233 visivyo na uchafuzi kwa mazingira katika ngazi ya mkoa na kitaifa, ikiongoza katika idadi ya mitambo ya kutengeneza chuma ambayo ni rafiki kwa mazingira nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha