

Lugha Nyingine
Uwekezaji wa China wa mali zisizohamishika katika reli wafikia dola za kimarekani bilioni 117.4 Mwaka 2021
Picha iliyopigwa Tarehe 18 Novemba 2021 ikionesha eneo la ujenzi wa reli ya mwendo kasi inayounganisha Miji ya Nanning na Yulin katika Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Cao Yiming)
BEIJING – Takwimu kutoka Shirika la Reli la Taifa la China zinaonesha kuwa, uwekezaji wa mali zisizohamishika wa China katika reli umefikia yuan bilioni 748.9 (sawa na dola za kimarekani bilioni 117.4) Mwaka 2021, kutokana na ujenzi wa njia nyingi za reli ulioanza katika kipindi hicho.
Mwaka 2021, jumla ya Kilomita 4,208 za njia mpya za reli zilianza kutumika kwa shughuli za uzalishaji, ikijumuisha kilomita 2,168 za reli za njia za mwendo kasi.
Hadi kufikia mwishoni mwa Mwaka 2021, urefu wa mtandao wa reli za mwendo kasi zinazotumika nchini China ulizidi Kilomita 40,000, huku miradi mikubwa ilianza kufanya kazi kama ilivyopangwa.
Sehemu ya reli ya mwendo kasi kati ya Miji ya Anqing na Jiujiang, ambayo ilianza kutumika wiki iliyopita, ni sehemu ya hivi karibuni kabisa ya reli kuanza kufanya kazi nchini China.
Kwa uzinduzi wa reli hiyo, sasa miji ya Hefei, Mji Mkuu wa Mkoa wa Anhui Mashariki mwa China, na Nanchang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Jiangxi wa China, imeunganishwa moja kwa moja na huduma za reli ya kasi.
Muda wa kusafiri kati ya miji hiyo miwili umepunguzwa hadi saa 2 na dakika 22.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma