Uongozi wa CPC wasikiliza na kupokea ripoti za utendaji kazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2022

BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wa kusikiliza na kupokea mfululizo wa ripoti za utendaji kazi.

Ripoti hizo zilizowasilishwa Alhamisi ya wiki hii, zimetoka kwa vikundi ongozi vya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC), Baraza la Serikali Kuu, Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China, Mahakama Kuu ya Umma, Idara kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya Umma, na vile vile kutoka Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC.

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, ameongoza na kuhutubia mkutano huo.

“Ili kukiongoza Chama chetu chenye wanachama milioni 95 na nchi yetu yenye watu zaidi ya bilioni 1.4, ni lazima tushikilie uongozi kamili wa Chama, hasa uongozi wa Kamati Kuu ulio madhubuti na wenye umoja,” inasomeka taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho.

Taarifa inasema kikao cha mwaka cha uongozi wa CPC cha kusikiliza taarifa za utendaji kazi kimekuwa mfano wa kushikilia uongozi kamili wa CPC pamoja na mamlaka ya Kamati Kuu ya chama hicho na uongozi wake ulio madhubuti na wenye umoja, na kubainisha kuwa mafanaikio hayo lazima yaendelee kwa muda mrefu.

Ikibainisha kwamba Mwaka 2021 ulikuwa wa kihistoria kwa CPC na nchi, mkutano huo umetambua mafanikio yaliyofikiwa na Bunge la Umma, Baraza la Serikali Kuu, Baraza la mashauriano ya kisiasa, Mahakama Kuu na Idara Kuu ya Mwendesha Mashtaka, pamoja na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC katika maeneo mbalimbali ya kazi.

Taarifa hiyo imesisitiza umuhimu wa Mwaka 2022 wakati China imeanza safari mpya ya kuelekea kutimiza lengo la karne ya pili tangu kuanzishwa kwa CPC Mwaka 1921 la kuiendeleza China kuwa nchi kubwa ya kisasa ya kijamaa ifikapo katikati ya Karne ya 21.

Vikundi ongozi vya wanachama wa CPC viliombwa kuendelea kuboresha uwezo wao wa kuamua na kuelewa masuala ya kisiasa na kutekeleza matakwa ya kisiasa, ili kuendana na Kamati Kuu ya CPC na Komredi Xi Jinping kwa mwelekeo mmoja katika msingi wake wa mawazo na kisiasa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha