China yasema imejizatiti kuonesha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Kuvutia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2022

BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema kwamba, nchi hiyo itaonesha kwa Dunia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ambayo ni ya kipekee na ya kuvutia, na kuwafanya washiriki wote kuhisi furaha na kuleta mshikamano, imani na nguvu zaidi duniani.

Wang Wenbin ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi ya wiki hii ambapo amebainisha kuwa katika siku ya kwanza ya kazi baada ya mapumziko ya Mwaka Mpya, Rais Xi Jinping wa China kwa mara nyingine tena alikagua maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022, tukio ambalo linadhihirisha kikamilifu umuhimu mkubwa unaopewa na China katika maandalizi hayo.

Wang amesema, kufuatia ombi la China kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kufanikiwa, watu wengi zaidi wa China wameshiriki katika michezo ya kuteleza kwa kasi kwenye barafu. Dhana iliyopendekezwa na China ya "kijani, umoja, wazi na safi" imetekelezwa vema katika ujenzi wa viwanja vya michezo hiyo, maandalizi na huduma za mashindano.

Amesema baada ya juhudi za miaka mingi, kazi ya China ya maandalizi ya michezo hiyo inakaribia kukamilika. Maeneo 12 ya mashindano huko Beijing, Yanqing na Zhangjiakou yote yamekamilika na yamepitishwa kwa kuidhinishwa na mashirika ya kimataifa ya michezo ya majira ya baridi.

Wang ameongeza kwamba, kwa upande wa huduma za michezo, Kijiji cha Olimpiki ya Majira ya Baridi, watu wa kujitolea, kituo cha vyombo vya habari, huduma za matibabu, hoteli na huduma nyingine zimetayarishwa kwa kutosha.

Akibainisha kuwa China ina imani ya kuandaa michezo ya Olimpiki kwa usalama licha ya janga la UVIKO-19, Wang amesema China itatekeleza hatua za kisayansi na sahihi za kuzuia na kudhibiti, kufanya kila iwezalo kuzuia kuzuka kwa janga hilo na kuhakikisha afya na usalama wa watu wote watakaoshiriki katika Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavua ya Majira ya baridi ya Beijing.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha