Mazungumzo ya pili ya maingiliano na maelewano ya ustaarabu yafanyika nchini China

(CRI Online) Januari 11, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Mazungumzo ya awamu ya pili ya maingiliano na maelewano ya ustaarabu yamefanyika Jumatatu ya wiki hii Beijing, Mji Mkuu wa China na kukutanisha watu 260 kutoka ndani na nje ya China, ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.

Michezo hiyo inachukua nafasi kubwa katika mazungumzo hayo, na washiriki wameeleza imani yao kuwa michezo hiyo itafanyika kwa mafanikio, na kusema Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itahimiza maingiliano ya utamaduni na kukusanya nguvu za mshikamano.

Balozi wa Misri nchini China Mohamed El-badri amesema, China imefanya juhudi kubwa katika kuandaa michezo hiyo kutokana na janga la UVIKO-19, na anaamini China inaweza kufanya Michezo hiyo kwa mafanikio.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha