Waziri wa Mambo ya Nje wa China Azungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahraini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2022

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahraini Abdullatif bin Rashid Al Zayani huko Wuxi, mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China Januari 11, 2022. (Xinhua/Ji Chunpeng)

Akisema kwamba China na Bahraini zina uhusiano wa muda mrefu na urafiki thabiti, Bw. Zayani amesema Bahraini inatia maanani kuimarisha na kukuza uhusiano wake na China, na ingependa kupanua ushirikiano wa pande hizo mbili katika sekta mbalimbali.

Bw. Wang alisema, China inathamini msimamo wa Bahraini wa kushikilia kufuata sera rafiki kwa China, na kushukuru uungaji mkono thabiti wa Bahraini kwa China katika masuala yanayohusu maslahi yake ya kimsingi na muhimu.

Bw. Wang alieleza kuwa China inashikilia kutetea na kufanya ushirikiano wa pande nyingi, kufuata nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, China siku zote inasimama kwenye upande wa nchi zinazoendelea na nchi ndogo na za ukubwa wa kati katika kulinda kwa pamoja haki na usawa wa kimataifa.

Bw. Zayani alisema, Bahraini inatambua kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa za kutoingiliana mambo ya ndani ya nchi nyingine, kuheshimiana, kuwa na ujirani mwema na kutatua migogoro kwa njia ya amani. Aliongeza kuwa, Bahraini pia inapinga kulifanya suala la haki za binadamu liwe la kisiasa, na kuunga mkono jitihada za China katika kulinda mshikamano na utulivu.

Bw. Zayani alisema, Bahraini inaunga mkono China kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na inapinga kuifanya michezo iwe ya kisiasa.

Pande hizo mbili pia zilibadilishana maoni juu ya ushirikiano kati ya China na Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba (GCC), suala la nyuklia la Iran na hali ya mambo katika Mashariki ya Kati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha