Wizara ya Mambo ya Nje ya China: China itaweka mazingira wezeshi kwa Waandishi wa Habari wa Nchi Zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2022

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Akijibu swali kuhusu wasiwasi uliooneshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchi za nje kuhusu kama uhuru wa vyombo vya habari kuandika habari wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing utaathiriwa na hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Januari 13 alisema, China kama kawaida italinda haki halali za waandishi wa habari na mashirika ya habari ya kigeni nchini China kwa mujibu wa sheria, na kuwezesha waandishi wa habari kuandika kwa urahisi habari za Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Bejing kwa mujibu wa mkataba wa mji mwenyeji wa michezo hiyo.

Wang alisema, China inatekeleza sera ya taifa ya kimsingi ya kufungua mlango. Mazingira ya vyombo vya habari vya nchi za nje kuripoti habari hapa China yamefunguliwa, na uandishi wa habari kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na mambo mengine husika ni huru. China ni nchi inayotawaliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni husika za sheria zimebainisha wazi haki halali na maslahi ya waandishi wa habari wa nchi za nje.

Alisema: “Tunakaribisha vyombo vya habari kufuatilia na kuandika habari kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na tunakaribisha maoni ya kiujenzi kutoka vyombo vya habari, lakini tunapinga vitendo vya kupotosha ukweli na kupaka matope China na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kwa kisingizio cha ‘uhuru wa habari’.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha