Kenya yazindua mfumo kielekroniki ili kuhimiza usalama wa chakula

(CRI Online) Januari 14, 2022

Kenya jana imezindua Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) wa kielektroniki utakaohimiza usalama wa chakula.

Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika nchini humo, Peter Munya amesema, Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) utawawezesha wakulima na wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo kuhifadhi mazao yao ili kupata stakabadhi za ghala (WR), ambazo zinaweza kufanyiwa biashara, kuuzwa, kubadilishana au kutumika kupata mikopo na pembejeo.

Bw. Munya amesema matumizi ya mfumo huo yanatarajiwa kupunguza hasara baada ya mavuno kutoka asilimia 40 hadi asilimia 10.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha