Rais wa Tanzania awaonya mawaziri kuhusu kuvuja kwa nyaraka za siri za serikali

(CRI Online) Januari 14, 2022

Rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan amewaonya mawaziri na maafisa wengine wakuu wa serikali kuhusu kile alichokiita kuwa ni kuvuja kwa nyaraka za siri za serikali.

Akizungumza kwenye kikao kazi na mawaziri na manaibu waziri mjini Dodoma jana, Rais Samia alieleza wasiwasi wake juu ya wimbi kubwa la uvujaji wa nyaraka za siri za serikali kwenye mitandao ya kijamii, akisema kwamba jambo hilo limekuwa kama ugonjwa.

Amewaelekeza mawaziri na wasaidizi wao kuziba mianya inayotumika kutoa taarifa za siri za serikali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha