China yasema baadhi ya nchi zapaswa kulaumiwa kimaadili kwa kuhodhi na kubadhirifu chanjo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2022

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin alisema Alhamisi ya wiki hii tarehe 13 kuwa ingawa idadi ya utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya konora imeongezeka duniani, watu wanaodungwa chanjo wameongezeka, lakini “pengo la kinga dhidi virusi vya korona” kati ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea bado linapanuka , na baadhi ya nchi zinapaswa kulaumiwa kimaadili kwa kuhodhi na kubadhirifu chanjo.

Katika mkutano na waandishi wa habari wa siku hiyo, mwandishi wa habari aliuliza kuwa, kwa mujibu wa ripoti, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema hivi karibuni kuwa, zaidi ya nchi 90 bado hazijafikia lengo la udungaji wa chanjo kwa asilimia 40 ya watu wote, na zaidi ya asilimia 85 ya watu wa Afrika bado hawajadungwa dozi moja ya chanjo hiyo. Tumeona kuwa balozi wa kukusanya mitaji ya Afya duniani wa WHO ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown, pia alisema kuwa baadhi ya nchi za Magharibi zina chanjo za ziada lakini bado zinalimbikiza , wakati nchi maskini zaidi zina upungufu mkubwa wa chanjo, na kitendo cha kulimbikiza chanjo kinapaswa kulaumiwa kimaadili. Upande wa China una maoni gani kuhusu kitendo hiki?

Wang Wenbin alisema kuwa China inaona kuwa kupambana na virusi vya korona ni jukumu la nchi zote. Chanjo dhidi ya virusi vya korona bado ni silaha kuu ya kupambana na virusi vya korona, na ni matumaini makubwa ya kuokoa maisha ya watu wengi zaidi.

Wang Wenbin alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu, katika nchi zenye mapato ya chini ni asilimia 5 ya watu tu ndiyo wamedungwa chanjo kikamilifu dhidi ya virusi vya korona. Barani Afrika, ni asilimia 7.5 ya watu bilioni 1.3 pekee wamedungwa chanjo hizo. Wakati huo huo, nchi chache za Magharibi zinahodhi chanjo ambazo zinazidi mahitaji yao wenyewe na chanjo nyingi zinatumiwa kwa ubadhirifu . Marekani pekee imebadhiri dozi zaidi ya milioni 15 za chanjo kati ya Mwezi Machi na Mwezi Novemba mwaka jana.

Alisema, kila mtu ana haki ya kuishi na haki ya kupata afya. Kutoa chanjo iwezekanavyo kwa Dunia hasa nchi zinazoendelea, na kujitahidi kuhimiza usambazaji wa haki wa chanjo hizo, hiki si kitendo cha ufadhili, bali ni jukumu. Aliongeza kuwa, Alieleza tumaini lake kuwa, nchi husika zinaweza kutimiza ahadi zao kihalisi, kufanya kazi pamoja na China kuziba "pengo la kinga dhidi ya virusi vya konora", na kutoa mchango unaostahiki kwa ajili ya ushindi wa mapema dhidi ya virusi vya korona. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha