Wanamichezo wa kuteleza kwenye theluji wa Iran wajawa na matumaini ya Olimpiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2022
Wanamichezo wa kuteleza kwenye theluji wa Iran wajawa na matumaini ya Olimpiki
Mshiriki mwenye matumaini ya kushiriki Michezo ya Olimpiki, Zahra Sulghani akiteleza kwa kasi kwenye theluji wakati wa shindano la kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Kuteleza kwenye theluji wa Hoteli ya Darbandsar huko Iran siku ya Jumapili ya wiki iliyopita (XINHUA)

TEHERAN- Huku Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ikikaribia, wanamichezo wa Iran wa kuteleza kwa kasi kwenye milima ya theluji ya Alpine wanawania nafasi ya kushindana kwenye jukwaa kubwa zaidi la michezo mjini Beijing.

"Natumai nitaweza kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing na ningependa sana kwenda China," anasema Fatemeh Kia Shemshaki mwenye umri wa miaka 17, mwanamichezo wa alpine ambaye anashiriki katika mashindano yanayoendelea ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki huko Iran kwenye Uwanja wa Kuteleza kwenye theluji wa Hoteli ya Darbandsar.

Kia Shemshaki amekuwa akiteleza kwenye theluji tangu akiwa na umri wa miaka 3 na alianza kushindana kwenye mashindano akiwa na umri wa miaka 11. "Washiriki wote wanafanya juhudi kubwa ili kufuzu kwa Olimpiki," anasema. "Natumai yeyote anayestahili anaweza kufuzu."

Mwingine mwenye matumaini, Zahra Sulghani mwenye umri wa miaka 21, pia amekuwa akiteleza kwenye theluji tangu akiwa na umri wa miaka 3, na anasema "mashindano yana kiwango cha juu sana na yana ushindani mkubwa sana".

"Ninatumai kuwa kila mtu atafaulu na wote wataweza kufikia matokeo wanayotamani," ameongeza.

Kama sehemu ya harakati zao za hivi karibuni za kufuzu kwa Michezo hiyo, wanamichezo maarufu wa Iran wameshiriki mashindano nchini Uturuki na katika hoteli za Tochal na Darbandsar za Iran. Wiki ijayo, wataelekea katika Hoteli ya Kimataifa yenye eneo la kuteleza kwenye theluji ya Dizin nchini humo.

"Licha ya ukosefu wa theluji ya kutosha, tuna mashine ya kutengenezea theluji huko Darbandsar, kwa hivyo tunaweza kuandaa mashindano ya kufuzu na kuwavutia watu kuteleza," anasema Mousa Saveh Shemshaki, Mkuu wa Kamati ya kiufundi ya Shirikisho la Mchezo wa Kuteleza kwenye Theluji la Iran.

Licha ya kuwa iko Asia Magharibi, Wairani wanapenda kuteleza kwenye theluji kutokana na milima ya nchi hiyo yenye theluji. Miongoni mwa watazamaji huko Darbandsar alikuwa Sahel Saveh Shemshaki mwenye umri wa miaka 15. Kazi yake kuu ni kutunza miteremko yenye theluji kabla na baada ya wanamichezo kumaliza kushindana, hali inayompa kijana huyo anayependa mchezo wa kuteleza kwenye theluji fursa ya kujifunza kutoka kwa wanamichezo walio bora zaidi nchini mwake.

"Ninapenda Olimpiki ya Majira ya baridi ya 2022 nchini China na ninavutiwa sana na Michezo hii," anasema. "Natumai kushiriki katika michezo kama hiyo katika siku zijazo."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha