Lugha Nyingine
Mwanafunzi kutoka Guinea-Bissau Ajitolea kwa jamii baada ya mlipuko wa Maambukizi ya Virusi vya Korona huko Tianjin
Evanilson akiongoza wakazi kusimama kwenye foleni katika makazi ya eneo la Dongli, Tianjin, Kaskazini mwa China Januari 15, 2022. (Picha/Xinhua)
Evanilson Gomes Alqueia kutoka Guinea-Bissau mwenye umri wa miaka 26 anasoma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tianjin. Baada ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya korona wa hivi karibuni huko Tianjin, Evanilson pamoja na rafiki yake wa kike kutoka Zimbabwe Kudzanai Dube wameajiriwa kama watoa huduma wa kujitolea kwenye jamii.
Evanilson amekuwa akifanya kazi za upimaji wa virusi vya korona, ambapo aliongoza wakazi kusimama kwenye foleni, kubeba vifaa vya huduma pamoja na wafanyakazi wa mitaa, na kusambaza maji ya moto kwa wafanyakazi ili kuondoa baridi.
“Ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona, tunatakiwa kubeba majukumu na kushirikiana kuvishinda.” Alisema Evanilson.
Evanilson akimpa kikombe cha maji ya moto mfanyakazi wa makazi ya eneo la Dongli, Tianjin, Kaskazini mwa China Januari 15, 2022. (Picha/Xinhua)
Evanilson akiongoza wakazi kusimama kwenye foleni katika makazi ya eneo la Dongli, Tianjin, Kaskazini mwa China Januari 15, 2022. (Picha/Xinhua)
Evanilson akiongoza wakazi kusimama kwenye foleni katika makazi ya eneo la Dongli, Tianjin, Kaskazini mwa China Januari 15, 2022. (Picha/Xinhua)
Evanilson akimpa kikombe cha maji ya moto mfanyakazi wa makazi ya eneo la Dongli, Tianjin, Kaskazini mwa China Januari 15, 2022. (Picha/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma