Tibet yakaribisha pilika za usafiri wa abiria kwa Treni ya “Fuxing” wakati wa Mwaka Mpya wa jadi wa China kwa mara ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2022

Saa mbili Asubuhi ya Januari 17, Treni ya “Fuxing” ilianza usafari wake wa kwanza wa abiria wa Mwaka Mpya wa jadi wa China kwenye Kituo cha Reli cha Lhasa,Tibet.

“Nimekuwa nikifanya kazi katika Mji wa Lhasa kwa miaka mitatu, hii ni mara yangu ya kwanza kupanda treni ya mwendo kasi kurudi nyumbani. Katika miaka michache iliyopita, muda wa kusafiri kwa basi kutoka Lhasa hadi Nyingchi ulihitaji zaidi ya nusu siku, lakini kwa sasa kupanda treni ya mwendo kasi muda huo unahitaji saa tatu na nusu tu, siyo tu unaokoa muda, bali pia ni salama zaidi. ” Dhondup kutoka Mji wa Nyingchi, Tibet alisema.

Mwezi Juni, Mwaka 2021, reli kutoka Lhasa hadi Nyingchi yenye urefu wa kilomita 435 ilizinduliwa na kuanza kazi ikiwa inaamaanisha kuwa Treni ya “Fuxing” tayari imefika mikoa na miji 31.  

Tangu kuzinduliwa kwa Reli ya Lhasa - Nyingchi,treni mbili za mwendo kasi na nyingine moja ya kawaida zimekuwa zikipishana kwenye miji kama vile Lhasa, Nyingchi, Shannan,na Shigatse, treni hizo zimewezesha usafari wa watu wanaoishi kwenye kando za reli hiyo. Kwa mujibu wa habari kutoka Kampuni ya Kundi la Reli ya Qinghai-Tibet la China, mwaandishi wa habari amefahamishwa kuwa hadi mwisho wa Mwaka 2021, Reli ya Lhasa - Nyingchi imesafirisha jumla ya abiria laki 6.21 na bidhaa zaidi ya tani 7900, na usafiri wa treni hiyo ya Fuxing umekuwa chaguo la kwanza kwa watu wanaoishi kwenye kando za reli hiyo.

Mkuu wa Kituo cha Reli cha Lhasa, Wang Fu alisema kuwa Mwaka Mpya wa jadi wa China wa 2022 ni wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa Reli ya Lhasa – Nyingchi. Inakadiriwa kwamba Kituo cha Lhasa kitasafirisha abiria 200,000 wakati wa Mwaka Mpya wa jadi wa China, na takriban abiria 5,000 kwa wastani kila siku.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha