Fedha za Yuani za China za Kidijitali za Matumizi ya Majaribio zafikisha miamala ya Yuan Bilioni 87.57

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2022

Mfanyakazi wa Benki ya Mawasiliano akionesha jinsi ya kutumia pochi ya mtandaoni ya e-CNY kwenye Bustani ya Huanlegu hapa Beijing, Mji Mkuu wa China. (Xinhua/Chen Zhonghao)

Fedha za Yuani za China za Kidijitali zimefikisha miamala ya Yuan bilioni 87.57 (dola za Marekani bilioni 13.78) hadi mwisho wa Mwaka 2021, huku China ikiongeza juhudi za utafiti na majaribio ya utumiaji wa fedha za kidijitali kwenye Benki Kuu.

Ofisa wa Benki ya Umma ya China Zhou Lan alisema Jumanne wiki hii kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, kwa jumla pochi binafsi milioni 261 za fedha za Yuani za China za Kidijitali zilifunguliwa, na sehemu za majaribio ya utumiaji wa fedha hizo zimezidi milioni 8.08.

Alisema, Benki Kuu ya China itaendelea kuhimiza utafiti na maendeleo ya majaribio ya utumiaji wa fedha za Yuani za China za kidijitali, na kuendelea kuimarisha majaribio ya utumiaji wa fedha za China za kidijitali katika biashara za rejareja, huduma za serikali na maeneo mengine kadha wa kadha.

Jitihada za China katika kuendeleza fedha za China za kidijitali ya Benki Kuu zilianza Mwaka 2014. Na kwa kufuata, Benki kuu ilifanya ushirikiano na Benki ya biashara na kampuni za mtandao wa intaneti katika utafiti na maendeleo kuhusu kazi husika kuanzia Mwaka 2017.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha