Upande wa China wamkaribisha Rais wa Poland kushiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2022

Kwa kujibu ripoti kuwa Rais wa Poland Andrzej Duda atashiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari Januari 19 kuwa China inamkaribisha kwa furaha Rais Duda wa Poland kuja China kushiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Hii imeonesha matumaini ya jumuiya ya kimataifa ya “kwenda pamoja kwa siku za baadaye”. “Pazia la Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing linakaribia kufunguliwa., China ina imani ya kufanya juhudi pamoja na pande zote katika kufuata moyo wa Michezo ya Olimpiki wa “kuwa na mshikamano zaidi” na kuionesha Dunia Michezo ya Olimpiki inayoandaliwa rahisi, yenye usalama na ya murua.” (Mwandishi wa Habari:Dong Xue)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha