

Lugha Nyingine
Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 yatoa Ripoti kuhusu urithi wa Michezo hiyo
Bustani ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, ambayo ni Makao Makuu ya kamati ya maandalizi ya michezo hiyo, kituo cha uendeshaji, ukumbi wa kuruka na kuteleza kwenye barafu wa Big Air wa Shougang na kumbi zingine za michezo. [Picha/Xinhua]
BEIJING - Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Beijing 2022 imetoa ripoti mfululizo za utafiti ambayo ina ripoti saba tofauti za urithi wa michezo hiyo zinazohusu mchango katika nyanja za michezo, uchumi, jamii, utamaduni, mazingira, maendeleo ya miji na maendeleo ya kikanda.
Utafiti wa urithi wa michezo hiyo unaangazia mchango wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na namna inawanufaisha watu wa China kabla ya kuanza kwa Michezo hiyo baada ya miaka mingi ya maandalizi kufuatia Beijing kushinda nafasi ya kuandaa michezo hiyo Mwaka 2015. Baada ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, urithi wa michezo hiyo utafaidika na maendeleo endelevu ya taifa.
"Ikiongozwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu, kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Beijing 2022 inaendelea kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu kwa njia isiyochafua mazingira, jumuishi, wazi na uadilfu," kamati hiyo imesema katika taarifa iliyotolewa pamoja na utafiti huo Jumatano ya wiki hii.
"Maandalizi ya Michezo yanaendelea kwa madhubuti na ahadi zimetekelezwa. Pamoja na kuzingatia Michezo hiyo na kujenga jukwaa kwa wanamichezo wa Dunia kushindana kwa haki na kuvunja rekodi, kamati ya maandalizi imeweka mkazo mkubwa katika uendelevu wa urithi."
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, urithi wa moja kwa moja wa Beijing 2022 ni ushawishi chanya wa Michezo ya Olimpiki kwenye maendeleo ya michezo ya majira ya baridi ya nchi hiyo. Ripoti inaonesha kwamba, idadi ya watu wa China ambao wameshiriki katika mazoezi ya michezo ya majira ya baridi, mashindano ya ridhaa au ya kitaaluma, na burudani za nje na za ndani zinazohusiana na michezo ya majira ya baridi imefikia milioni 346, na kupita lengo la milioni 300 lililowekwa wakati Beijing iliposhinda nafasi ya kuandaa michezo hiyo.
Ripoti hiyo ya michezo inasema Shughuli za Taifa za Msimu wa Barafu na Theluji zimefanyika kwa miaka 7 nchini China tangu Mwaka 2014, huku shughuli hiyo ya mwaka huu imeanza mwezi uliopita wa Desemba 2021 na litaendelea hadi Aprili, 2022.
Katika shughuli ya mwaka huu ya Msimu wa Barafu na Theluji, michezo ya majira ya baridi na matukio mengine ya burudani ya barafu na theluji yanahimizwa kwa sekta zote za jamii. Zaidi ya matukio 4,700 kama haya yamefanyika tangu Mwaka 2014.
Ripoti hizo zimetoa mifano mingi kuonesha juhudi za Kamati ya Olimpiki ya Beijing 2022 za kuliacha Taifa la China na urithi mkubwa wa Olimpiki. Ikijumuisha matumizi endelevu ya majumba ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, maendeleo ya teknolojia ya 5G katika mji mwenyeji mwenza wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 wa Zhangjiakou mkoani Hebei, na ulinzi wa wanyama pori huko Yanqing, kitongoji cha Beijing ambacho ni mojawapo ya maeneo matatu ya mashindano ya michezo hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma