Mpiga picha akibeba mkoba wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008 katika kituo cha vyombo vya habari cha Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2022

Huku zikiwa zimebaki siku chini ya 30 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, baadhi ya waandishi wa habari wameonekana katika kituo cha vyombo vya habari cha michezo hiyo wakibeba mikoba ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Beijing 2008 ambayo waandishi wa habari walipewa bure.

Mpiga picha wa Iran alisema anabeba mkoba huo kila akipiga picha kwenye mashindano ya michezo.

"Kwa sababu ubora wake ni mzuri sana," mpiga picha alisema, na " ulisanifiwa mahsusi kwa ajili ya wapiga picha."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha