Timu ya Olimpiki ya Kanada yatazamia medali kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2022

Mwanamke akiteleza kwenye theluji. (Picha inatoka IC.)

Mengi yanatarajiwa kutoka kwa Timu ya Olimpiki ya Kanada ya kuteleza kwenye theluji wakati Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inapokaribia.

Timu hiyo iliyotangazwa Jumatano ya wiki hii, inatarajiwa kuwa "timu yenye nguvu zaidi katika timu zote za mchezo wa kuteleza kwa ubao kwenye theluji".

Timu hiyo ya Kanada ambayo ilishinda medali nne kwenye Michezo ya Olimpiki ya Pyeongchang 2018, inatazamia kuendeleza rekodi hiyo kwani washindi wote wanne waliopita -Sebastien Toutant, Max Parrot, Mark McMorris na Laurie Blouin wamerudi tena kushindania medali.

Toutant, mshindi pekee wa medali ya dhahabu, atatetea medali yake ya dhahabu katika mchezo wa kuteleza kwenye barafu na kuruka juu kwa wanaume na pia atashindana kwa mtindo wa mteremko.

Orodha ya wachezaji wa Timu ya Kanada yatangazwa

Siku ya Jumatatu ya wiki hii, wachezaji 16 (wanawake wanane na wanaume wanane) wa mchezo wa mbio za kuteleza kwenye barafu kwa njia ndefu waliteuliwa kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022.

Kanada imeshinda jumla ya medali 37 za Olimpiki katika mchezo wa mbio za kuteleza kwa kasi kwenye barafu kwa njia ndefu ikiwa ni zaidi ya medali ambazo nchi hiyo imeshinda katika mchezo mwingine wowote kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Timu ya wanawake wanne na wanaume watatu imeteuliwa kuiwakilisha Kanada katika mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji, huku ikiwa na wachezaji wanaorejea katika Olimpiki Cendrine Browne na Dahria Beatty kwenye kikosi cha wanawake.

Timu ya mchezo wa magongo ya wanawake (hockey) italenga kupata medali yake ya tano ya dhahabu kwa jumla na ya kwanza tangu Mwaka 2014 itakapofungua pazia la kusaka medali kwa kupambana na Timu ya Uswizi Feb 3.

"Ni heshima kubwa na mafanikio kuchaguliwa kuwakilisha nchi yako kwenye Michezo ya Olimpiki," Tom Renney, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mchezo wa Magongo nchini Kanada amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha