Rais wa Zanzibar aunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ya Mwaka 2022

(CRI Online) Januari 24, 2022

(Picha inatoka ukurasa wa akaunti ya Facebook ya Rais Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.)

Rais Zanzibar nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kupitia mitandao ya kijamii kuwa anaunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, na kuitakia mafanikio makubwa michezo hiyo.

Rais Mwinyi amesema anaitakia mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ya 2022. Amesema Michezo ya Olimpiki ni tukio kubwa la michezo kwa watu wote duniani, kwa hivyo haipaswi kuingizwa mambo ya siasa, na inapaswa kuepushwa na siasa. Amesema, ni kupitia kuheshimu moyo wa Olimpiki na kutohusishwa na mambo ya siasa, ndipo tunaweza kutimiza umoja wa kimataifa na kauli mbiu ya Olimpiki: kasi zaidi, juu zaidi na wenye nguvu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha