Kampuni 10 bora za China kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu ya UN (SDGs)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2022

Kwa mujibu wa ripoti ya Kampuni 100 za Kibinafsi za China kwa maendeleo endeleovu iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti ya Hurun Januari 10 mwaka huu, kampuni kubwa ya maziwa ya Yili ya China inaongoza katika orodha ya kampuni 100 za China Bara ambazo zinaendana na Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

Ripoti hiyo iliangazia kampuni 100 zilizoorodheshwa katika Kampuni za kibinafsi 500 zenye thamani kubwa kwa Mwaka 2020 chini ya Taasisi ya utafiti wa Hurun ya China, na nafasi hiyo inatokana na ripoti zao za kimazingira, kijamii na utawala, ripoti za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, na ripoti za malengo ya maendeleo endelevu.

Kati ya kampuni 100, 31 ziko katika eneo la Delta ya Mto Yangtze, 25 katika Eneo la Ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macao, 17 mjini Beijing, 14 mjini Shenzhen, na 11 huko Shanghai.

Sasa, hebu tuangalie kampuni 10 bora kutoka China zinazoenda sambamba na malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

 


No. 8 (kufungana) Kampuni ya GEM

Sanamu iliyotengenezwa kwa chuma ikiwa imesimama katika kampuni ya kuchakata taka ya GEM huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, Agosti 26, 2021. [Picha/IC].

 


No 8 (kufungana): Tencent

Mwanasesere mwenye taswira ya pengwini anaonekana kumwangalia mwanamke katika banda la Kampuni ya Tencent wakati wa maonesho huko Shanghai. [Picha na Fan Jianlei/China Daily]

 


No. 8 (kufungana): BYD

 Wageni wa maonesho wakitazama magari yanayooneshwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Mwaka 2021 ya Magari ya Chongqing Mwezi Juni. [Picha na Zhang Dandan/China Daily]

 


No. 7: Alibaba

Nembo ya Kampuni ya Alibaba ikionekana wakati wa Tamasha la manunuzi la Tarehe 11 Novemba katika makao makuu yake huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Novemba 11, 2020. [Picha/Mashirika]

 


No. 4 (kufungana): Kampuni ya Fosun

Watu wakitembelea Banda la Kampuni ya Fosun kwenye maonesho huko Shanghai, Novemba 5, 2021. [Picha/IC]

 


No. 4 (kufungana) Kampuni ya Bima ya Pingan

Jengo la Kampuni ya Bima ya Pingan huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Desemba 5, 2021. [Picha/IC]

 


No. 4 (kufungana) Kampuni ya Haier

Banda la Maonesho la Kampuni ya Haier katika Maonesho ya Dunia ya Vifaa na Elektroniki ya 2021 huko Shanghai Mwezi Machi. [Imetolewa kwa China Daily]

 

No. 3: Kampuni ya Country Garden

Mchoro wa kubuni wa mradi uliojengwa na Kampuni hiyo mjini Foshan, Mkoa wa Guangdong. [Picha/bgy.com.cn]

 

No. 2: Huawei

Wanunuzi wakijaribu HarmonyOS katika duka kuu la Huawei huko Shanghai. [Picha /Long Wei, China Daily]

 

No. 1: Kampuni ya Yili

Msichana akiangalia bidhaa za Yili. [Picha kwa hisani ya Tovui ya Yili]

 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha