Chuo Kikuu cha China chafanya utafiti na utengenezaji wa Roboti ya Kuteleza kwenye Theluji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2022

Siyo tu wachezaji hodari wanaweza kushiriki kwenye michezo ya kuteleza kwenye theluji, bali pia roboti zinaweza kufanya vizuri katika michezo ya majira ya baridi. Roboti yenye miguu sita iliyotengenezwa na watafiti wa China imeshateleza kwenye mteremko.

Roboti hiyo iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Jiao Tong cha China, ilifanya majaribio mbalimbali ya kuteleza kwenye theluji katika uwanja wa mbio za theluji mapema mwezi huu huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa Kaskazini Mashariki mwa China.

Roboti hiyo inafanana na mbwa, ikiunganishwa miguu minne ili kusimama imara, na pia ina miguu mingine miwili inayoshika nguzo mbili za kusaidia kuteleza kwenye theluji.

Watafiti wa chuo hicho walisema, licha ya kupima uwezo wake kwenye mbio za kuteleza kwenye theluji, pia wataitumia roboti hiyo katika kazi za kufanya doria na uokoaji kwenye milima ya theluji, ili kujenga mazingira salama kwa wachezaji wa kuteleza kwenye theluji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha