China yatimiza malengo ya mazingira safi Mwaka 2021

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2022

Picha iliyopigwa kutoka angani Agosti 4, 2021 ikionesha Kituo cha Uzalishaji wa Umemenuru cha Kijiji cha Tujing, Mji wa Datong, Mkoa wa Shanxi, China. (Xinhua/Cao Yang)

Ofisa wa Serikali ya China amesema Jumatatu wiki hii kwamba, mwaka jana China imetimiza malengo yake kwa mazingira ikiwa imepunguza uchafuzi kwa mazingira na kuendelea kuboresha kiwango cha usafi wa maji na hewa.

Msemaji wa Wizara ya Mazingira na Mazingira ya Asili Liu Youbin kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, China imetimiza malengo yote manane iliyojiwekea yanayohusu utoaji wa carbon dioxide na kiwango cha ubora wa maji juu ya ardhi.

Maendeleo ya China katika kupunguza utoaji wa carbon dioxide kwa kipimo cha GDP ya kila mtu yamefikia malengo ya Mpango wa 14 wa maendeleo ya Miaka Mitano (2021-2025). Upunguaji wa machafuzi ya aina nne kuu, ikiwemo oxynitride pia umefikia malengo ya mwaka.

Licha ya hayo, China iliripoti kiwango bora cha usafi wa maji ya juu ya ardhi mwaka jana. Mito na Maziwa yaliyofikia daraja la kwanza hadi tatu imefikia asilimia 84.9, ikidhihirisha hali ya mazingira ya asili inaendelea kuboreshwa. Ubora wa maji ya juu ya ardhi unagawanywa katika madaraja matano nchini China, na daraja la kwanza ndilo la kiwango cha juu zaidi cha ubora.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha