Mazingira Bora ya biashara nchini China yatambuliwa kote Duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2022

BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema kwamba, juhudi za China za kupanua ufunguaji mlango wa uchumi na kuboresha mazingira ya kufanya biashara zimepata mafanyikio makubwa na kutambuliwa na kampuni za kigeni.

Zhao Lijian amesema hayo Jumatatu ya wiki hii wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya tafiti za hivi karibuni kuhusu imani ya kampuni za kigeni kwa soko la China.

Kwa mujibu wa "Utafiti wa Imani ya Biashara" wa kila mwaka ulifanywa na kutolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Ujerumani nchini China na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu na ushauri ya KPMG, kampuni za Ujerumani nchini China kwa sasa zina matumaini kuhusu ukuaji wa soko la China.

Akibainisha kuwa kuimarika kwa uchumi wa Dunia kunakabiliwa na changamoto huku kukiwa na janga la UVIKO-19, Zhao amesema kuwa China inaendelea kutoa mchango katika uchumi wa Dunia na ukuaji endelevu na thabiti wa uchumi wake.

Amesema China imedhamiria kujenga uchumi wa Dunia ulio wazi na mazingira ya biashara ya kimataifa kwa msingi wa kanuni za soko na sheria, na kutoa uhakikisho mkubwa kwa kampuni za kigeni kuwekeza na kufanya biashara nchini China.

Zhao amedokeza kuwa Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira ya Kufanya Biashara ya Mwaka 2020 inaiweka China katika nafasi ya 31 duniani kwa urahisi wa kufanya biashara, na ameongeza kuwa nafasi hiyo ya China katika Mwaka 2012 ni 91.

"Hii inaonesha mazingira ya kufanya biashara ya China yameboreshwa kwa kiasi kikubwa," amesema msemaji huyo.

Amesema China itaendelea kujitolea kufungua mlango kwa kiwango cha juu, kugawana fursa za maendeleo na Dunia, na kufanya utandawazi wa kiuchumi uendelezwe kwa mwelekeo wa wazi zaidi, unaojumuisha watu wote, wenye uwiano na wenye manufaa kwa wote.

"China itajiunganisha zaidi katika soko la kimataifa na kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine," Zhao amesema na kuongeza kuwa China itashirikiana na pande nyingine kujenga uchumi wa Dunia ulio wazi na kuweka msukumo mkubwa katika kufufua uchumi wa Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha