Tanzania yazindua programu ya sayansi ya roboti ili kuhimiza maendeleo ya teknolojia

(CRI Online) Januari 25, 2022

Chuo Kikuu cha Dodoma Tanzania na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wamezindua program mpya itakayotoa elimu kuhusu sayansi ya roboti ili kuhimiza teknolojia hiyo nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa programu hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano Bw. Mohamed Khamis Abdullah, amesema programu hiyo itaanzishwa kwa kuwekwa maabara ya sayansi katika chuo kikuu hicho.

Ameondoa hofu iliyopo kwamba kuingizwa kwa roboti kunaweza kuwa tishio kwenye suala la ajira, akisema teknolojia hiyo itasaidia kuendeleza mageuzi ya kidigitali. Pia amesema teknolojia hiyo itachochea maendeleo ya sekta mbalimbali kama vile kilimo na afya.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Bw Emmanuel Luoga, amesema programu hiyo itatoa mchango kwa maendeleo ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha