EU yasema iko tayari kukabiliana na Russia kama diplomasia itashindwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2022
EU yasema iko tayari kukabiliana na Russia kama diplomasia itashindwa
Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama, akihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja huo mjini Brussels, Ubelgiji, Januari 24, 2022. Umoja wa Ulaya (EU) umejiandaa kukabiliana dhidi ya mashambulizi yoyote ya mtandaoni ya Russia au vitisho mseto ikiwa itavamia Ukraine na "imeendelea sana" katika maandalizi yake ya kukabiliana na uchokozi wowote, mwanadiplomasia mkuu wa EU, Josep Borrell, amesema hapa Jumatatu. (Xinhua/Zheng Huansong)

BRUSSELS - Umoja wa Ulaya (EU) uko tayari kujilinda dhidi ya mashambulizi yoyote ya mtandaoni ya Russia au vitisho mseto iwapo itaivamia Ukraine na "imeendelea sana" katika maandalizi yake ya kukabiliana na uchokozi wowote, Mwanadiplomasia Mkuu wa EU, Josep Borrell, amesema.

Amewaambia waandishi wa habari mapema wiki hii kufuatia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwa, umoja huo umeungana katika mtazamo wake.

"Jeshi la Russia ndani na karibu na Ukraine na majaribio ya Russia kuunda upya mipaka katika bara letu inadhoofisha misingi na kanuni za msingi ambazo usalama wa Ulaya umejengwa na kurudisha kumbukumbu za giza za nyanja za ushawishi, ambazo hazifai katika Karne ya 21," Borrell amesema.

Amesema kuwa EU imethibitisha uungaji mkono wake kamili na usio na shaka kwa Ukraine na kwamba uvamizi wowote wa kijeshi dhidi ya Ukraine utakuwa na madhara makubwa na gharama kubwa kwa Russia.

Amesema mawaziri hao wa mambo ya nje walikuwa na mazungumzo marefu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Borrell amesema kuwa juhudi za pamoja za kidiplomasia zitaendelea kuishawishi Russia kuchukua njia ya mazungumzo "ingawa kauli za Russia hazileti imani kubwa."

Ameitaka Russia kuendelea kushirikiana na washirika wake wa kimataifa kueleza na kukanusha habari zisizo sahihi, yaani "muktadha hatari unaoenezwa."

"Iwapo diplomasia itashindwa, tumeendelea sana katika maandalizi yetu ya kukabiliana na uvamizi wowote wa Russia. Hakika, itakuwa hatua ya haraka na thabiti siyo tu ndani ya EU lakini pia kimataifa," amesema.

Mapema Jumatatu, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alitangaza kwamba Baraza Kuu la EU linataka kuipatia Ukraine bajeti mpya ya msaada wa kifedha ili kuisaidia kukabiliana na mgogoro uliopo sasa kati yake na Russia.

Uhusiano kati ya Ukraine na Russia ulizorota hivi majuzi, huku pande zote mbili zikipeleka idadi kubwa ya wanajeshi na vifaa katika maeneo ya mpakani.

Marekani, Ukraine, na NATO zimeishutumu Russia kwa kukusanya Vikosi vya Kijeshi na vifaa vya kivita karibu na mpaka wa Mashariki wa Ukraine, kwa nia inayowezekana ya "uvamizi." Russia imekanusha shutuma hizo ikisema kuwa ina haki ya kuwakusanya wanajeshi ndani ya mipaka yake ili kulinda eneo lake kwani shughuli za NATO ni tishio kwa usalama wa mpaka wa Russia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha