Tanzania yakabidhiwa msaada zaidi wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kutoka China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 27, 2022

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu wakisalimiana kwa viwiko kwenye hafla ya kukabidhiana chanjo dhidi ya virusi vya korona kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Januari 26, 2022. (Picha ilipigwa na Herman Emmanuel/Xinhua)

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian alikabidhi shehena ya chanjo dhidi ya virusi vya korona kutoka China kwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Baada ya kukabidhwa chanjo hizo waziri huyo wa Tanzania aliishukuru China kwa kutoa msaada kwa wakati. Alisema chanjo hizo zitasaidia kuongeza kasi ya kampeni ya kudunga chanjo nchini Tanzania ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona.

Na pia alisema, dozi hizo laki 8 za chanjo dhidi ya virusi vya korona za Sinopharm zitadungwa kwa watu laki 4, na aliongeza kuwa, shehena ya kwanza ya chanjo za Sinopharm laki 5 iliyotolewa na China Novemba, 2011 ilidungwa kwa watu laki 2.5.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu wakishiriki hafla ya kukabidhiana chanjo dhidi ya virusi vya korona kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Januari 26, 2022. (Picha ilipigwa na Herman Emmanuel/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha