

Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya China yasifu sana uungaji mkono wa Rais Putin wa Russia kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alisema Januari 26 kuwa upande wa China unasifu sana uungaji mkono wa Rais Vladimir Putin wa Russia kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Ameeleza matumaini yake kuwa wanamichezo wa nchi mbalimbali wakiwemo pamoja na wanamichezo wa Russia watapata mafanikio bora na kung'ara kwenye uwanja wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.
Rais Putin wa Russia alisema Januari 25 kuwa Russia na China zote zinapinga kulifanya suala la michezo liwe suala la kisiasa, zinapinga kitendo cha kususia michezo kilivyo kama kuonesha “mchezo wa kufurahisha” , na kufuata kithabiti moyo wa Michezo ya Olimpiki wa kutetea usawa na haki. Siku hiyo hiyo, Balozi wa Russia nchini China Andrey Denisov alisema kwamba Russia itatuma ujumbe wa wanamichezo wengi kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na anaamini kuwa michezo hiyo itapata michezo mafanikio makubwa.
“Upande wa China unasifu sana uungaji mkono wa Rais Putin wa Russia kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.” Zhao Lijian alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, China na Russia, sawa na nchi nyingi duniani, zinapinga kulifanya suala la michezo liwe suala la kisiasa,na siku zote zinafuata kwa makini moyo wa Michezo ya Olimpiki wa “ kushikamana na kupendana, kufanya ushindani kwa haki, na kuelewana”.
“ Bado zimebaki siku 9 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Natumaini wanamichezo wa nchi mbalimbali wakiwemo pamoja na wanamichezo wa Russia watapata mafanikio bora na kung'ara kwenye uwanja wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.” Zhao alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma