

Lugha Nyingine
Afisa Mwandamizi wa CPC atoa wito kwa vyombo vya habari vya kimataifa kutoa habari za Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022
BEIJING -- Afisa Mwandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Kunming Jumatano ya wiki hii ameelezea matumaini yake kwamba marafiki kutoka vyombo vya habari vya kimataifa watashiriki kutoa habari chanya za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing na kuonesha Michezo hiyo ya Olimpiki ya "kuvutia, ajabu na bora".
Huang Kunming, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China (CMG).
Likiwa na mada ya "Pamoja kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi yenye Teknolojia ya Juu," kongamano hilo liliandaliwa na CMG na kusimamiwa kwa pamoja na Kamati ya Olimpiki ya China na Kamati ya Maandalizi ya Beijing ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi na ya Walemavu ya 2022.
Huang amesema China iko tayari kutoa huduma za kina, zenye ufanisi na zinazofaa kwa vyombo vya habari kutoka nchi zote.
Huang ameelezea matarajio yake kwamba vyombo vya habari vya kimataifa vitakuza kwa pamoja mazingira yasiyo na upendeleo, ya haki na ya afya na kusaidia kukuza maingiliano kati ya watu duniani kote.
Wawakilishi wa mashirika 145 ya vyombo vya habari kutoka nchi na kanda 78, pamoja na wale kutoka mashirika ya kimataifa, walishiriki kwenye kongamano hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma