Mwenyekiti wa UNECA asifu Mafanikio ya Uuzaji wa Kahawa ya Ethiopia nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 28, 2022

(Picha inatoka CFP.)

Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) ilisema, mafanikio ya uuzaji wa kahawa ya Ethiopia nchini China ya hivi karibuni yatakuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za Afrika katika kutumia ipasavyo uwezo wao wa kuuza bidhaa katika masoko ya kimataifa.

"Mafanikio ya uuzaji wa kahawa ya Ethiopia nchini China yatatoa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine kumi za Afrika ambako ECA inafanya kazi mwaka huu, kutoa uwezo mkubwa zaidi wa kuuza bidhaa za Afrika nchini China", taarifa iliyotolewa na ECA kwa Shirika la Habari la China, Xinhua, ikimnukuu Vera Songwe Naibu Katibu Mkuu wa UN ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa ECA ilisema.

"Tunafurahi sana kushirikiana na Serikali ya Ethiopia katika fursa hiyo ya uhakika, kuona namna gani uhusiano huo wa kiwenzi utaboresha hali ya maisha ya Waethiopia, kwa kutoa jukwaa la kufanya biashara kwa pande mbili", alisema Songwe.

Takwimu kutoka UNECA zinaonesha, kwenye mkutano wa kuzindua uuzaji wa chapa za kahawa ya Ethiopia uliofanyika katika jukwaa kubwa zaidi la biashara tovuti ya mtandaoni ya China, Alibaba (Tmall Global) wiki iliyopita, zaidi ya mifuko 11,200 ya kahawa ya Ethiopia iliuzwa ndani ya sekunde chache chini ya jitihada za pamoja za ECA na Serikali ya Ethiopia.

"Uzinduzi huu umethibitisha siyo tu Ethiopia, bali pia bara la Afrika linaweza kunufaika na utumiaji wa mfumo wa kidigitali", taarifa ya ECA ilinukuu kauli ya Waziri wa Biashara na Ushirikiano wa Kikanda wa Ethiopia, Gebremeskel Chal.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha