Habari Picha: Rais Xi asherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China na watu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 28, 2022

Tangu 2013, kila mwaka kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China, Rais wa China Xi Jinping amekuwa akifanya ziara za ukaguzi kote China na kutoa salamu za Mwaka Mpya kwa watu wa makabila yote.

2013

Rais Xi Jinping akimhudumia chakula mzee alipotembelea mkahawa katika nyumba ya kuwahudumia wazee huko Lanzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Gansu Kaskazini-Magharibi mwa China, Februari 4, 2013. (Xinhua/Lan Hongguang)

2014

Rais Xi Jinping akiwapa watoto zawadi za Mwaka Mpya wa jadi wa China katika Nyumba ya Watoto Yatima ya Hohhot, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani nchini China, Januari 28, 2014. Xi alifanya ziara mkoani Mongolia ya Ndani na kutoa salamu za Mwaka Mpya kwa watu wa makabila yote. (Xinhua/Lan Hongguang)

2015

Rais Xi Jinping (katikati) akiwatembelea watu katika Kijiji cha Liangjiahe, Kitongoji cha Wen'anyi katika Wilaya ya Yanchuan, Yan'an, Mkoa wa Shaanxi Kaskazini-Magharibi mwa China, Februari 13, 2015. Xi alitoa salamu za Mwaka Mpya kwa wenyeji katika maeneo vituo vya zamani vya mapinduzi na kwa Wachina wa makabila yote kote nchini. (Xinhua/Lan Hongguang)

2016

Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Jiangxi Mashariki mwa China kuanzia Tarehe 1 hadi 3 Februari 2016, siku chache kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Xi ametoa salamu za mwaka mpya kwa raia na wanajeshi wote wa China. Rais Xi Jinping (wa tatu kutoka kushoto) akitengeneza mkate kwa kuponda wali pamoja na wanakijiji wa Jinggangshan, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, Februari 2, 2016. (Xinhua/Lan Hongguang)

 

2017

Rais wa China Xi Jinping (katikati) akitembelea nyumba ya mwanakijiji Xu Wan katika Kijiji cha Desheng, Kitongoji cha Xiaoertai cha kaunti ya Zhangbei, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Januari 24, 2017. Xi alihimiza kuongeza juhudi za kupunguza umaskini wakati wa ziara ya kukagua Mji wa Zhangjiakou. (Xinhua/Lan Hongguang)

2018

Rais Xi Jinping wa China akizungumza na wanavijiji na wajumbe wa kikosi kazi cha kukabiliana na umaskini alipotembelea nyumba ya familia maskini katika Kijiji cha Sanhe, Sanchahe katika kaunti ya Zhaojue, eneo linalojiendesha la kabila la Wayi la Liangshan, katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China Februari 11, 2018. (Xinhua/Ju Peng)

2019

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akitembelea nyumba za wakazi katika eneo la Qianmen katikati mwa Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 1, 2019. Rais Xi Jinping alitembelea wakazi na maafisa wa ngazi ya msingi mjini Beijing na kutoa salamu za Mwaka Mpya kwa watu wa makabila yote ya China. (Xinhua/Ju Peng)

2020

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akipiga ngoma ya mbao ya kabila la Wawa mara tatu ili kubariki mwaka mpya katika Kijiji cha Sanjia katika Mji wa Tengchong, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, Januari 19, 2020. (Xinhua/Ju Peng)

2021

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akizungumza na wanavijiji wanaoshiriki katika shughuli za sikukuu, na kutoa salamu zake za mwaka mpya kwa watu wa makabila yote kote nchini, kwenye uwanja wa umma wa Kijiji cha Huawu, Kaunti ya Xinren ya kabila la Wamiao, Mji wa Qianxi, Bijie, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Februari 3, 2021. Xi alikagua Mkoa wa Guizhou wa Kusini-Magharibi mwa China kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China. (Xinhua/Xie Huanchi)


(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha