Rais wa China Xi Jinping aahidi mchango mkubwa wa China katika kulinda amani duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2022

Picha iliyounganishwa ikimuonesha Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, akizungumza kwa njia ya video na askari wa kulinda amani wa China waliotumwa nje ya nchi wakati wa ukaguzi wa Eneo la kati la Jeshi la Ukombozi la Umma (PLA) Januari 28, 2022. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amewataka askari wa kulinda amani wa China kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kulinda amani ya Dunia wakati wa ukaguzi wa eneo la kati la Jeshi la Ukombozi la Umma (PLA) siku ya Ijumaa wiki hii.

Akiongea kupitia njia ya mtandao na askari wa kulinda amani wa China waliotumwa nje ya nchi, rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, amewataka waimarishe tahadhari za usalama na kuongeza kinga na udhibiti wa UVIKO-19 huku kukiwa na mazingira yasiyotabirika.

Xi ametoa salamu za Sikukuu ya Spring, Mwaka Mpya wa jadi wa Kichina kwa askari wa PLA na Jeshi la Polisi la Umma, wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi kwenye majeshi, na wanamgambo na vikosi vya akiba.

Akisifu mafanikio yaliyopatikana na eneo la kati la PLA, Xi amesisitiza kwamba misheni zote zinapaswa kukamilishwa kwa ubora na hatua lazima zipigwe katika maendeleo na utayari wa vita.

Akisema kuwa Sikukuu ya Spring na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing viko karibu, Xi ametoa wito kwa vikosi vyote vya jeshi kujiandaa kila wakati kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa na utulivu wa kijamii wa China.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa maafisa na wanajeshi wakati wa ukaguzi wa eneo la kati la Jeshi la Ukombozi la Umma (PLA) Januari 28, 2022. (Xinhua/Li Gang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha