

Lugha Nyingine
Rais Xi kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022
Mwenge wa Olimpiki kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 ukioneshwa kwenye Mnara wa Olimpiki huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Oktoba 20, 2021. (Xinhua/Wang Yong)
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Hua Chunying ametangaza Ijumaa ya wiki hii kwamba, kuanzia Februari 4 hadi 6, Rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, na kufanya hafla ya kuwakaribisha wakuu wa nchi mbalimbali duniani, wakuu wa serikali, wajumbe wa familia za kifalme na wakuu wa mashirika ya kimataifa watakaohudhuria sherehe hiyo, na kufanya shughuli mbalimbali husika za uhusiano wa pande mbili.
Kwa mujibu wa Hua, viongozi hao wa kimataifa ni pamoja na Rais wa Russia Vladimir Putin, Mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni, Rais wa Singapore Halimah Yacob, Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Zhaparov, Rais wa Tajikistani Emomali Rahmon, Rais wa Turkmenistan Gurbanguly Berdymukhamedov, Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Mwanamfalme wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Poland Andrzej Duda, Rais wa Serbia Aleksandar Vucic, Mfalme Henri wa Luxembourg, Mwanamfalme wa Monaco Albert II, Rais wa Argentina Alberto Fernandez, Rais wa Ecuador Guillermo Lasso, Waziri Mkuu wa Mongolia Luvsannamsrai Oyun-Erdene, Waziri Mkuu wa Pakistani Imran Khan, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Bosnia na Herzegovina Zoran Tegeltija, Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini Park Byeong-seug, Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan Ali Ahmadov, Binti Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulla Shahid, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani Daren Tang, Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo Marcos Troyjo, na Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) Zhang Ming.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma