Beijing yashuhudia kupungua kwa idadi ya visa vya ndani vya UVIKO-19

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2022
Beijing yashuhudia kupungua kwa idadi ya visa vya ndani vya UVIKO-19

BEIJING - Serikali ya Mji wa Beijing, Mji Mkuu wa China siku ya Ijumaa imetoa taarifa ya kuonesha kuwa kwa sasa mlipuko wa virusi vya korona umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwani maambukizi mapya yanapungua na yako miongoni mwa wakazi ambao tayari wamewekwa karantini.

Xu Hejian, Msemaji wa Serikali ya Mji wa Beijing amesema, kuanzia saa 10 mchana Alhamisi hadi saa 10 mchana Ijumaa wiki hii, Beijing imeripoti visa vipya vinne vya maambukizi ya ndani ya virusi vya korona vinavyohusiana na kirusi cha korona aina ya Delta. Hakuna maambukizi mapya ya kirusi aina ya Omicron ambayo yameripotiwa kwa siku tano mfululizo.

Mji wa Beijing umefungua vituo vingi zaidi vya upimaji wa UVIKO-19 katika sehemu za wakazi walio hatarini kupata maambukizi, na kuimarisha upimaji na kupuliza dawa ya kuua virusi kwenye vyakula vya baridi vilivyoagizwa kutoka nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha