CMG yafanya mahojiano na Rais wa Russia

(CRI Online) Februari 04, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Mkuu wa Shirika kuu la Utangazaji la China (CMG) ambaye pia ni mhariri mkuu wa Shirika hilo Bw. Shen Haixiong amefanya mahojiano na rais wa Russia Vladmir Putin kabla ya rais huyo kuja Beijing kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022.

Katika mahojiano hayo, Rais Putin amesema, China imekamilisha maandalizi yote kwa ajili ya michezo hiyo, na imewekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu ya michezo na mawasiliano. Pia China imejenga majumba na viwanja vya kisasa vya michezo, na kuweka mazingira mazuri ya usalama wa wanamichezo, makocha na waandishi wa habari kutoka nchi za nje.

Amesisitiza kuwa, Russia inapinga kuingiza mambo ya siasa kwenye michezo, na kupinga kutumia michezo kuwa mbinu za kushinikiza, kushindana bila usawa, na ubaguzi.

Amesema anaamini michezo hiyo itakuwa ya kiwango cha juu zaidi katika historia, na anawatakia wanamichezo wote kushiriki kwenye mashindano bila vikwazo na kupata matokeo mazuri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha