

Lugha Nyingine
Michezo ya 24 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yafunguliwa
(CRI Online) Februari 04, 2022
Sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya 24 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imefanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa taifa wa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametangaza kufunguliwa kwa michezo hiyo.
Wakuu wa mashirika ya kimataifa wakiwemo mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Bw. Thomas Bach, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, na viongozi wa zaidi ya nchi 30 akiwemo rais Vladmir Putin wa Russia wameshiriki kwenye ufunguzi huo.
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni michezo mikubwa ya kwanza inayofanyika kama ilivyopangwa tangu kutokea kwa mlipuko wa janga la COVID-19, na inawashirikisha wanamichezo karibu 3000 kutoka nchi takriban 90. (Picha: Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma