Rais wa Olimpiki wa Uganda: China itaandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi yenye mafanikio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2022

KAMPALA - Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Uganda (UOC) Donald Rukare amesema kuwa China itaandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2022 yenye mafanikio.

"Sote tunajua mazingira mazuri ya China kuandaa mashindano ya Dunia yenye mafanikio makubwa. Nina matumaini kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 itaratibiwa vema na kufanikiwa sana," Rukare ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano maalum Ijumaa ya wiki iliyopita.

Amesema inafurahisha kuona China ikiandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi baada ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Mwaka 2008 kwa mafanikio.

"Tunatazamia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi nchini China yenye mafanikio na ya kuvutia zaidi," amesema.

Amesema UOC ilimuunga mkono mwanamichezo Brolin Mawejje ili aweze kushiriki mashindano hayo ya majira ya baridi, lakini ilikuwa ni bahati mbaya alishindwa kufuzu baada ya majaribio.

"UOC tungependa kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing," Rukare amesema.

Siyo nchi nyingi kutoka Afrika zinazoshiriki Olimpiki ya Majira ya baridi. Katika bara hili, ni wanamichezo wa Eritrea, Ghana, Madagascar, Morocco, na Nigeria pekee ndiyo wanaoshiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha