Washiriki kutoka nchi mbalimbali wapongeza sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2022

Fashifashi zikimulika angani usiku wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing wa Kiota cha Ndege, Februari 4, 2022. (Xinhua/Li Xin)

BEIJING - Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imeanza rasmi Februari 4, na sherehe za ufunguzi, ikiwa ni sehemu ya kufunguliwa kwa pazia la Michezo hiyo, zimesifiwa na kupongezwa na washiriki wa kimataifa.

Sherehe hizo zikipambwa na maonesho ya mwanga wa kuvutia na fashifashi za kustaajabisha, zilivutia wajumbe kutoka nchi na sehemu 91 duniani waliokusanyika katika Uwanja wa Taifa, au tuseme ni Kiota cha Ndege, kushuhudia Mji wa Beijing, Mji Mkuu wa China ukiwa mji wa kwanza kabisa kuandaa kwa mara mbili Michezo ya Olimpiki yaani ya majira ya joto na ya baridi.

"Sote tulitazamia kwa hamu kubwa sherehe ya kusisimua ya ufunguzi. Ni tofauti sana lakini inasisimua kama Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Beijing 2008," Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Thomas Bach, ambaye alijumuika na umati wa watu na kutazama sherehe hiyo iliyoshirikisha takriban watoa burudani 3,000.

"Ni maonesho makubwa, na ni maboresho makubwa ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008," ameshangaa Gianni Merlo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Wanahabari wa Michezo. Alivutiwa na sherehe ya shangwe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Beijing 2008, na akipongeza sherehe hii mpya ya majira ya baridi iliyofanyika kwa muda mfupi.

Wasanii wakitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, Februari 4, 2022. (Xinhua/Chen Yichen)

Akiwa ameketi miongoni mwa wanahabari wa vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali duniani, Masaru Komatsu anayefanya kazi katika Shirika la Uchapishaji la Michezo la Tokyo alikuwa akishika simu yake ya mkononi mara kwa mara ili kupiga picha matukio ya ajabu ya sherehe za ufunguzi.

"Ingawa kuna baridi sana usiku wa leo hapa Beijing, ninaweza kuhisi shauku ya watazamaji kwenye uwanja wa michezo, na nitaandika habari kuhusu msisimko wa sherehe ya ufunguzi" alisema kijana huyo wa miaka 30. "Ninapenda usanifu wa kutumia fashifashi kwa kuhesabu muda kuelekea ufunguzi wa michezo, na fashifashi za rangi ya bluu na kijani zinaonekana kuangaza msimu wa baridi."

Maarten Delvaux, mwandishi wa habari kutoka Ubelgiji ambaye aliripoti Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Tokyo na baadhi ya matukio ya soka ya kimataifa, amefurahi kuona maonesho ya sherehe ya ufunguzi moja kwa moja, huku Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 ikiwa ya kwanza kwake kushuhudia na ziara yake ya kwanza nchini China.

"Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Beijing 2008 ilikuwa na sherehe kubwa ya ufunguzi," Delvaux amesema. "Hii ni ndogo kidogo, lakini naona inaangazia zaidi mambo ya utamaduni wa China."

Wasanii wakitumbuiza kabla ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, Februari 4, 2022. (Xinhua/Yang Lei)

Wanamichezo wa nchi na sehemu mbalimbali duniani walipita mbele ya hadhara kwenye sherehe hiyo, wakiongozwa na wasanii wa China ambao walikuwa wakicheza pembezoni, na Claudia Pechstein, mmoja wa wanamichezo wenye mafanikio zaidi wa Ujerumani, alijivunia kubeba bendera ya Ujerumani huku kukiwa na shangwe kubwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha