Je Mwanamichezo huyu asiyevaa shati alihisi baridi au la?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2022

Kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, mshika bendera wa Samoa ya Marekani Nathan Crumpton hakuhofia baridi na alionekana katika mwili wake uliotiwa mafuta bila kuvaa shati, alivaa sketi ya nyasi na makubadhi. Baada ya sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo, alipewa jina la "mshika bendera aliyeganda zaidi kwa baridi katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi" na watazamaji wa China na wa kigeni.

Ujumbe wa Samoa ya Marekani ukiingia uwanja wa kufanyia sherehe ya ufunguzi jioni ya Februari 4. (Xinhua/Mpiga picha: Ju Huanzong)

Mchana wa Tarehe 7, mwanamichezo huyu wa kiume wa kuteleza kwenye theluji kwa kutumia kigari cha chuma alionekana kwenye Kituo cha Taifa cha kuteleza kwenye theluji kwa kutumia kigari na sleji. Kuhusu "watu wa mtandao wa internet kuwa na wasiwasi kama alihisi baridi au la," Crumpton aliwaambia waandishi wa Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba alikuwa akifanya mazoezi siku hizi na hakufuatilia sana maoni ya kwenye mtandao. “lakini ni kweli mikono yangu inahisi baridi sana! Mikono yangu ilishika nguzo ya bendera ilikuwa ikihisi baridi sana. Sehemu nyingine ziko sawa, kwa kuwa nilihisi baridi kwa muda mfupi tu .”

Crumpton alisema kuwa sketi ya nyasi na mapambo aliyovaa yote ni mavazi ya jadi yenye historia ndefu, na alitumaini kutumia fursa ya kushiriki kwenye michezo hiyo kuonesha utamaduni na upenzi wa mavazi hayo.

Crumpton alisema kuwa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ni za murua. Ingawa wakati aliposubiri kuingia kwenye uwanja hakuweza kuona sherehe za ufunguzi za kipindi cha kwanza, lakini mara aliporudi chumbani tu alitazama kwenye TV, “sherehe za ufunguzi zilikuwa nzuri kweli, na pia ni zisizoweza kusahauliwa.”

Crumpton alisema kuwa anashukuru sana kwa hali ya kujali kutoka kwa watazamaji wa China na wa nchi nyingine mbalimbali na anatumaini kulipa kila mtu kwa kupata mafanikio mazuri kwenye michezo hiyo.

Uzoefu wa kibinafsi wa Crumpton ni mkubwa sana. Crumpton mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya, na sasa anaishi katika Mji wa Park wa Jimbo la Utah, Marekani, na amewahi kuishi katika nchi za Uswizi, Zimbabwe na Australia.

Kwenye tovuti yake binafsi, Crumpton anajitambulisha kuwa ni mwanamichezo, mwanamitindo na mpiga picha. Pamoja na kuteleza kwenye theluji kwa kutumia kigari cha chuma, anapenda mpira wa raga , mpira wa magongo, riadha ya kwenye theluji na kuteleza kwenye theluji. Mwaka 2021 alishiriki pia kwenye mchezo wa riadha kwa mbio za mita 100 kwa wanaume kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Tokyo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha